Loading...

STURRIDGE AUMIA MAZOEZINI, KUKAA NJE TENA KWA MUDA ZAIDI

 Daniel Sturridge
Huku akiwa amekaribia kupona majeraha yake ya awali, mshambuliaji mwingereza wa Liverpool Daniel Sturridge amejiumiza tena na hivyo kukosekana katika mechi ijayo ya Kombe la Ligi dhidi ya Stoke City.
Sturridge a,echeza mechi sita tu msimu huu huku akicheza 19 kwa msimu uliuopita kufuatia kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara jambo linalomuumiza kichwa kocha mpya wa timu hiyo, Jurgen Klopp.
Klopp sasa amebakiwa na chaguo moja tu la straika, Christian Benteke kwa sababu Daniel Ings na Divock Origi pia wanasumbuliwa na majeraha.
Sturridge hajacheza tangu aumie dhidi ya Newcastle December 6 mwaka jana na baada ya ushindi wa siku ya Boxing Day dhidi ya Leicester City alitweet kuwa amerudi mazoezini na hali yake iko vizuri.

ZIDANE APEWA MIKOBA YA BENITEZ REAL MADRID

 Zinedine Zidane (left) and president Florentino Perez
Nguli wa soka ambaye alitengeneza jina akiwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, Zinedine Zidane ameteuliwa rasmi kuiongoza klabu hiyo kufuatia kutimuliwa kwa Mhispania Rafael Benitez kufuatiua mwenendo mbovu wa timu hiyo toka achukue kiti hicho.
Benitez, 55 amekua na msimu mbovu na Real Madrid ikiwemo uhusiano wake na staa wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo jambo lilioanza kuonyesha dalili mbaya za siku za Benitez klabuni hapo.
Benitez ametimuliwa baada ya kikao cha bodi kilichokaa jana Jumatatu na kuamua kumpa majukumu mchezaji huyo wa zamani wa Ufaransa na mshindi wa Kombe la Dunia la 1998.
Zidane, 43 ameonyesha kufurahia uteuzi huo huku akisema ni furaha ya pekee kufundisha klabu kubwa kama Real Madrid yenye historia ya pekee Ulaya.
Zidane ataanza kazi rasmi Jumamosi hii ambapo ataivaa Deportivo la Coruna jkatika dimba la Bernabeu huku akiwa ni kocha wa 11 kuteuliwa katika kipindi cha miaka 12 ya utawala wa Rais Florentino Perez klabuni hapo.
Benitez amepoteza michezo mitatu tu kati ya 25 huku akiipeleka Real katika hatua ya 16 bora kwenye Klabu Bingwa Ulaya. Ushindi wa 8-0 dhidi ya Malmo na ule wa 10-2 dhidi ya Rayo Valecano ni miongoni mwa mechi za kukumbukwa za kocha huyo akiwa Madrid. 
Kuondoka kwa Benitez kunaweza kuwa kumechangiwa na masuala kadhaa ikiwemo kipigo cha aibu kutoka kwa mahasimu wao wakuu Barcelona cha 4-0 pale Bernabeu jambo linalosemekana kuzua ugomvi katio yake na staa wa timu hiyo, Ronaldo. 
Zidane anapewa mikoba hiyo  huku Florentino akigoma kusema mkataba waliompa nguli hiyo aliyekua kwenye benchi la ufundi la Team B ya Real Madrid.

RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA WIKIENDI HII IKO HAPA

Sat 2 Jan 2016 - Premier League
  • West Ham v Liverpool 12:45
  • Arsenal v Newcastle 15:00
  • Leicester v Bournemouth 15:00
  • Man Utd v Swansea 15:00
  • Norwich v Southampton 15:00
  • Sunderland v Aston Villa 15:00
  • West Brom v Stoke 15:00
  • Watford v Man City 17:30
Sun 3 Jan 2016 - Premier League
  • Crystal Palace v Chelsea 13:30
  • Everton v Tottenham 16:00
Tue 12 Jan 2016 - Premier League
  • Aston Villa v Crystal Palace 19:45
  • Bournemouth v West Ham 19:45

KIPA SUNDERLAND ATOA MSAADA WA EURO 5,000 KWA VIZIWI.

 Jack Butland


Kipa wa Stoke City, Mwingereza Jack Butland ametoa Euro 5,000 kwa ajilim ya timu ya Taifa ya Wanawake  Uingereza ya Viziwi ili waweze kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ya Viziwi nchini Italy June mwaka huu.
Butland aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa amejifunza mengi sana kutoka kwenye michuano mikubwa na amepata uzoefu mkubwa kwahyo alitaka kuwasaidia nao wapate uzoefu huo.
Pamoja naye, wachezaji wengine wa Kiingereza Lucy Bronze, Jade Moore, Jo Potter na Fran Kirby wamechangia ili kufanikisha jambo hilo huku kiwango kinachohitajika ni Euro 20, 000.
Butland, ambaye amecheza mechi tatu na England, pia ni balozi wa kampeni ya ubaguzi wa rangi ya Kick Out Discriminatio.

UNITED YAANDAA PAUNI 35mil KUMPATA ANDERSON

Man Utd set to offer Lazio £35m for Felipe Anderson 
Manchester United inajiandaa kutuma ofa ya pauni mil 35 kwa ajili ya kupata huduma ya mchezaji wa Lazio, Mbrazil Felipe Anderson ambaye anakipiga Lazio nchini Italia. United inatarajia kufanya uhamisho huo kuwa wa kwanza katika dirisgha dogo la usajili lililofunguliwa rasmi leo.
Anderson, 22 anasakwa na United ambayo inahaha baada ya kucheza michezo 8 bila ya ushindi jambo linalomlazimisha Ed Woodward kufanya kazi ya kumfatilia mbrazili huyo ili kuimarisha kikosi chake.
Hii si mara ya kwanza kwa United kumfukuzia mchezaji huyo, mara baada ya Van Gaal kupewa kazi Old Trafford alifanya juhudi kumnasa ikashindikana lakini kufuatia fomu mbaya ya kikosi hicho inawalazimu kumnunua Anderson.
Van Gaal na Ed Woodward walishuhudia timu hiyo ikitumia karibu Pauni 100 milioni katika kiangazi kilichopita lakini wako tayari kuvunja benki tena kufanya usajili kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo imehangaika kuliona lango msimu huu.
Mazungumzo baina ya timu hizo yameanza siku 10 zilizopita huku United wakiwa tayari kulipa milioni 25 kupata saini ya mchezaji huyo wa zamani wa Santos ambaye amecheza mechi yake ya kwanaza na Brazil June mwaka 2015.

Licha ya Anderson kukosa uzoefu wa timu ya Taifa lakini United ina imani kuwa mchezaji huyo atawafaa mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu ya Uingereza.

 

VAN GAAL; NASTAAFU BAADA YA KAZI UNITED

Van Gaal: Manchester United job could be my last  

Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amekiri kuwa baada ya kuifundisha timu hiyo atafikiria kustaafu rasmi kazi hiyo. Van Gaal amekana kuhusu uamuzi huo kuhusishwa na mwenendo wa klabu hiyo inayosua sua baada ya kucheza michezo nane bila ya ushindi wowowte katika michuano yote huku akiishuhudia timu hiyo ikishuka hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
 Droo iliyopatikana dhidi ya Chelsea wiki hii jumatatu ilipunguza presha kwa kocha huyo baada ya kupokea vipigo vitatu mfululizo kutoka kwa Bournermouth, Norwich City, Stoke City jambo lililozua shaka juu ya kibarua cha Mholanzi huyo aliyekua kocha wa Uholanzi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazili kiangazi cha 2014.
United itavaana na Swansea wikiendi hii huku Van Gaal akiwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya kikosi hicho, ameshindwa kuifunga timu hiyo katika mechi zote tatu walizokutana akiambulia vipigo tu.
Jina la Jose Mourinho linatajwa sana kwenye midomo ya mashabiki wa timu hiyo jambo linaloonyesha kuchoshwa na falsafa ya Mholanzi huyo. Kwenye mechi dhidi ya Chelsea muuzaji wa bidhaa za Manchester Ubited nje ya uwanja wa Old Traford alionekana amebeba skafu zenye rangi nyekundu na jina la Mourinho jambo linaloonyesha mwisho wa Mholanzi huyo unakaribia huku bodi ya timu hiyo ikiendelea kumvumilia.


Newer Posts
© Copyright +255 ONLINE | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top