Loading...

ZOUMA NJE MIEZI SITA

 Kurt Zouma


Beki wa klabu ya Chelsea, Mfaransa Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kufika miezi sita kufuatia jeraha la goti alilopata katika mechi ya weekend hii dhidi ya Manchester United.
Zouma aliumia goti lake wakati akigombea mpira na kiungo wa United Michael Carrick na madaktari wamethibitisha atalazimika kufanyiwa upasuaji.
Katika akaunti yake ya Twiter Zouma alithibitisha kuumia kwa goti lake na kwamba upasuaji utafanyika muda wowote hivi karibuni huku akiwashukuru watu wote ambao wamekua wakimtumia message za pole.
Kwa maana hiyo Mfaransa huyo atakosa michuano ya Ulaya ambayo itafanyikia nchini kwake hapo baadae June akiwa ameshacheza mechi mbili za timu ya Taifa toka aitwe kwa mara ya kwanza.
Wachezaji mbalimbali wameendelea kumtumia salamu za pole na kumtakia pone haraka huku wakiongozwa zaidi na wachezaji wa Ufaransa.
Kiungo wa United, Morgan Schneiderlin aliandika katika ukurasa wake wa Instagram "Pole sana kwa kuumia, natumaini utarudi tena ukiwa imara zaidi".
Zouma lijiunga na Chelsea akitokea klabu ya St Ettiene ya Ufaransa katika dirisha la mwaka 2014 na ametengeneza ukuta mzuri pamoja na mkongwe John Terry ambae amethibitisha kuiacha klabu hiyo baada ya msimu huu.

MOURINHO AFANYA MAZUNGUMZO NA MABOSS WA MANCHESTER UNITED

Jose Mourinho and Louis van Gaal 


Uongozi wa klabu ya Manchester United umefanya mazungumzo na wawakilishi wa Kocha aliyeachwa na Chelsea, Jose Mourinho.
Mourinho, 53 aliefukuzwa na Chelsea mwezi Desemba ana matumaini makubwa ya kupata kibarua hicho akimrithi Louis van Gaal ambaye amekua na wakati mgumu Old Trafford kufuatia kiwango hafifu cha timu hiyo kwa miezi ya karibuni.
Hakuna maelewano rasmi yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili na klabu haijatoa taarifa yoyote rasmi lakini kuna kila dalili akapata dili hilo huku ujio wa kocha Pep Giardiola ukiongeza hamasa ya Morinho kubakia England ili apambane na hasimu wake wa zamani akiwa Real Madrid.
Van Gaal anajiandaa kuiacha klabu hiyo baada ya msimu huu, ikiwa ni msimu mmoja tofauti na ilivyotarajiwa kama mkataba wake unavyosema.
Hii inatoa picha kuwa Mourinho ndiye mrithi pekee wa Van Gaal baada ya msimu huu. Mreno huyo hajafanya mazuzngumzo na klbau yoyote toka aachie ngazi Stamford Bridge na United haijawasiliana na kocha yeyote toka Manchester United iwe na matokeo mabovu ikiwemo kutolewa kwenye Michuano ya klabu bingwa Ulaya, UEFA.


That would leave the way clear for Mourinho, who is known to be excited by the prospect of taking over at Old Trafford.


WANAJESHI 120 WAUAWA NCHINI SYRIA

 Syrian woman fleeing embattled city of Aleppo in Bab al-Salam, next to the city of Azaz. 5 Feb 2016


Mapambano makali yameibuka jirani na mji wa Allepo kaskazini mwa Syria wakati majeshi ya Serikali yakijaribu kuwazunguka waasi waliojificha katika mahandaki.
Kundi la Wachunguzi wa Haki za Binadamu la Syria limesema wanajeshi zaidi ya 120 kutoka katika pandezote mbili wameuawa kwenye mji wa Ratyan Ijumaa hii.
Zaidi ya wakimbizi 20, 000 walikimbia mapigano yanayoendelea wakijaribu kuvuka mpaka wa Syria kuelekea nchini Uturuki.
Uturuki imesema imejiandaa kuwasaidia wakimbizi ingawa mipaka imefungwa. Siku chache zilizopita majeshi ya Syria yalisaidiwa msaada wa silaha za anga na majeshi ya Urusi katika mji wa Allepo.
Ijumaa hii televisheni ya Taifa ya nchini Syria ilisema majeshi ya waasi yaliuteka mji wa Ratyan ulioko kaskazini kidogo mwa mji wa Allepo.
Newer Posts Older Posts
© Copyright +255 ONLINE | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top